Matumizi-binafsi
Matumizi-binafsi ni moja ya mabadiliko ya msingi kwenye taswira tuliyonayo ya nishati, kuondoka kutoka kwenye mifumo ya kati na kuwa na mifumo iliyotawanyika, ambayo haitegemei gridi, lakini kwa wakati huo huo kila wakala anaweza kuwa mtoaji/muuzaji wa nishati.
Matumizi-binafsi yanawezekana kufanyika kwa mawakala wote: Watu binafsi, biashara, viwanda, miji, na yoyote anaweza kushiriki kwa viwango tofauti kiurahisi tu kwa kufunga vifaa vya kuzalisha kutegemea na mazingira ya eneo husika.
Uzalishaji wa umeme kutoka katika vyanzo mbadala ni rahisi sana na una faida, pia inakupa nafasi ya kuchangia kufanya dunia iwe endelevu na uweze kukidhi matumizi yako binafsi.
Kipengele kingine ni uhifadhi wa nishati, ambacho ni muhimu kama vile tu uzalishaji wenyewe kwa sababu inatuwezesha kuwa na usalama na kuwa na nishati muda wote.