Majengo janja
Majengo janja ni majengo yaliyounganishwa kwa kiwango kikubwa na yaliyobuniwa ili kutumia rasilimali kikamilifu. Kuanzia katika ubunifu mpaka utendaji kazi wake, ufanisi mkubwa katika matumizi ya nishati na katika kutumia nafasi umefikiriwa. Faida zake ni nyingi sana.
Ufanisi katika nishati, uzalishaji endelevu na matumizi kamilifu ya rasilimali za kiteknolojia ni vitu muhimu sana katika majengo janja. Kwa kufanya mifumo mingi iweze kujiendesha ndani ya majengo, inawezekana kuokoa nishati na maji kwa kupitia vumbuzi za kiteknolojia.
Kwa upande mwingine, kufanya mifumo kujiendesha kunawezesha majengo kuwa kama wateja wa nishati ambayo yanaizalisha, hivyo kuitumia katika majengo binafsi, na kwa upande mwingine, kurudisha nishati ya ziada katika gridi. Uunganishwaji unafanya iwezekane kukusanya taarifa nyingi za kuchambua na kurekebisha ufikishwaji wa nishati katika mifumo mbalimbali ya jengo, hivyo kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali na kuepoka upotevu. Taarifa za aina nyingi zinakusanywa na ni jambo linalofanywa sana siku hizi kwani inawezesha kutambua hali ya kiafya ya watu au usambaaji wa virusi au maambukizi.
Mifumo ya BMS au Building Management Systems inawezesha kutazama na kutafsiri makundi ya taarifa ili kuboresha ubora wa maisha ya watu wanaotumia jengo au kuishi ndani yake. Kuanzia paneli za sola zilizotumika kama kuta za jengo na hifadhi ya nishati mpaka programu za utambuzi wa sura (facial recognition) na upimaji wa joto, vitu vyote ni sehemu ya dhana ya Jengo Janja. Wachoraji wa ramani za majengo wana nafasi kubwa sana katika ufanisi wa matumizi ya rasilimali, kwa sababu itapunguza matumizi ya viyoyozi, vifaa vya kuongeza joto na umeme kwa kutumia faida asili inayopatikana katika nafasi husika.